Unordered List

Definition List

Picha Mpya Toka Kwa Harusi Ya Kimye: Andrea Bocelli, Msanii Kipofu Aliyeambiwa Akalale Baada Ya Shoo Yaibuka

Picha nyingine kutoka harusi kubwa zaidi kutokea ya Kimye yaibuka.

E! imeachilia picha hii ikimuonyesha Andrea Bocelli akipiga shoo mbele ya Kim na Kanye mwezi jana tarehe 24.

Msanii huyu ambaye huimba nyimbo za Opera inaaminika siku hio aliimba nyimbo ya "Con te partirĂ²," inayomaanisha kwa Kiswahili 'nikiwa na wewe wakati wote nitakutoka'.


Kwa maana nyingine ni kuwa 'nitakuwa na wewe milele' ndio maana Kim na Kanye waliweza kuoana.

Kando na hapo wawili hao waliweza kufanya harusi mbele ya ukuta uliotengenezwa na maua kwa mkono (katika hio picha).

E! wameongezea kuwa Andrea Bocelli aliweza pia kuimba nyimbo ya "Ave Maria" wakati Kim alipokuwa akipanda jukwaani akiwa ameshikwa mkono na babake Bruce Jenner.

Sijui kwa nini picha ya Andrea Bocelli iliweza kuachiliwa kwa uharaka lakini tunavyojua ni kuwa habari kutoka kwa New York Post zinadai kuwa Andrea, ambaye pia ni kipofu aliweza kudhalilishwa kwa harusi hio kwa kufanya shoo akiwa amesimama bila kupewa kiti na baada ya hapo kuingizwa kwa gari na kuambiwa aende nyumbani kulala.

Pia ripoti zaidi ni kuwa Jaden Smith alikuwa amelewa kupindukia na kuanza kuvunja chupa na kujizungukia ovyo kama mtu mwendawazimu.

Cheki Full report ya yaliyotendeka kwa harusi ya Kimye kulingana na New York Post

Madai hayo yote si official lakini official ni kuwa tuna baadhi ya picha kutoka harusi ya Kim Kardashian-Kanye West
Picha Mpya Toka Kwa Harusi Ya Kimye: Andrea Bocelli, Msanii Kipofu Aliyeambiwa Akalale Baada Ya Shoo Yaibuka Picha Mpya Toka Kwa Harusi Ya Kimye: Andrea Bocelli, Msanii Kipofu Aliyeambiwa Akalale Baada Ya Shoo Yaibuka Reviewed by Admin on Saturday, June 07, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.