IMEBAINIKA kuwa wapo baadhi ya wasanii wa filamu na muziki nchini Tanzania kuwa na tabia ya kujipiga picha za uchi na kuzitumia visivyo ikiwemo kuzituma kwenye mitandao hali inayochangia mmomonyoko wa maadili nchini.
Sakata la kusambaa kwa picha hizo zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za watu maarufu nchini leo limeibuka tena bungeni likiwa na sura mpya huku baadhi ya wabunge wakitaka kujua serikali inachukua hatua gani juu ya picha zilizosambaa juzi zinazomuonesha mmoja wa wabunge akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alikanusha na kudai si za kwake.
Moto huo ulizidi kuwaka bungeni leo katika kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Mchinga (CCM), Mhe. Said Mtanda ameihoji serikali wamechukua hatua gani dhidi ya vitendo vya uchapaji wa picha zisizozingatia maadili huku akiwataja Wema na Diamond kupiga picha wakiwa chumbani na kuweka kwenye mitandao.
Katika majibu yake Naibu waziri Habari Utamaduni na Michezo Mheshimu Mkamia, alijibu kuwa serikali imebaini juu ya matumizi hayo ya picha.
Mheshimiwa Habib Mnyaa aliuliza swali la nyongea kwa wizara ya mawasiliano ya sayansi na teknolojia ambapo jibu hilo lilijibiwa na waziri wa mawasiliano.
Katika majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka.”

Wabunge Wachafuka!! Wataka Hatua Za Mastaa Kupiga Picha Za Uchi Kushtakiwa
Reviewed by Admin
on
Tuesday, June 10, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano