Unordered List

Definition List

Mistari 10 Ya Kutongoza Mwanamke Mara Ya Kwanza Unayofaa Kuiacha


'Kuna yule mwanamke jirani nimemzimia na leo atakiona kuwa mi ni mbabe katika haya maswala ya kusuka demu.'

Haya ni baadhi ya maneno wanaume wengi huyatumia kujipa morale ya kutongoza mademu, lakini je huwa unayapima maneno yako mara ya kwanza unapomzukia mwanamke ambaye hujawahi kumtongoza?

Inabainika kuwa midume mingi hukosa zare lao kwa mademu kwa sababu ya kutowaridhisha kimistari wanawake. Na sababu kuu ni kutumia mistari hafifu kiasi cha kuonekana wakumbavu ama kutojali mbele ya mademu.

Cheki mistari 10 ambayo hufai kamwe kutumia kabisa ukiwa wamshobokea mwanamke mara ya kwanza.

10. Kwani wee ni Miss Universe? Wafanya Modelling Wapi?
Makosa hapa hufanyika sababu ni kuwa utamfanya mwanamke kukufikiria kuwa wafikiria kuwa mamodels ndio wanawake wazuri pekee. Mwanamume mjanja hafai kuutumia huu mstari mara ya kwanza kwani demu utakaye muuliza hata fikra zake labda hazipo kwa modeling. Labda anaweza kuwa nesi, mwalimu, secretari nk.

9. Nakupenda
Ni makosa kumwambia unampenda mwanamke mara ya kwanza unapomtongoza. Demu atakufikiria kuwa wewe una nia mbaya na yeye, na zaidi atakufananisha wewe kama kijana mdogo ambaye hujielewi.
Huwezi kumpenda mtu na siku ya kwanza halafu umwambie hapo hapo. Lazima taratibu flani zifuatwe.

8. Mamako lazima atakuwa ni gaidi manake duh! wewe ni kama bomu
Huu ni stari mzuri kwa mara ya kwanza kuleta gumzo kwa mwanamke lakini sahizi na mambo na alshaabab, bokoharam na alqaeeda haifai. Hakuna mtu angetamani kuhusishwa na mambo ya kigaidi.

7. Una Makalio mazuri kuliko hata ya Masogange
Labda pekee uwe unatongoza mwanamke kwa danguro, huu mstari hauufai kuutumia kwingine. Mstari huu mwanamke anaweza kuumaanisha 'nimependa mwili wako na nataka kulala na wewe.'

6. Hallo darling
Kuna baadhi ya maneno siku hizi yanatumiwa ndivyo sivyo. Wapata watu wanaitana madarling, mabeby, na masweetheart bila mpangilio wowote. Hapo hakuna shida lakini demu ukianza kumuita darling siku ya kwanza lazima akushuku. Atakuona wee umepotoka kwani maneno hayo hutumika kwa watu specially ambao wawafahamu vyema maishani na si hivi hivi tu.

5. Mteme mshkaji wako uje kwangu
Mambo na kukazana kuwa lazima demu aachane na jamaa lake ili awe wako si issue poa kabisa. Kuna midume mingine wanapenda kujaribu kula chakula cha wengine bila kutoa jasho.
Kama wee ni mwanamume aina hii halafu demu kama huyo anaongea na wewe basi ujue anasoma level yako ya akili na hakuna chochote kati yenu kitakachofanyika. Si rahisi demu kuachana na jamaa lake kwa urahisi hivyo.

4. Lazima peponi kuna malaika aliyepotea
Huu ni mistari uliotumika kabla mababu zetu kuzaliwa. Na kama utautumia kwa demu mara ya kwanza atakuona ubunifu wako akilini uko sufuri.

3. Mambo vipi kabinti karembo
Jinsi utakavyotumia maneno yako kumridhisha mwanamke kuna maana kuu sana. Ukijifanya sharobaro siku ya kwanza atakuona sharobaro milele.

2. Niko hapa kukusaidia
Unayemwambia kuwa uko hapo kumsaidia labda wewe ndiye uliyejaa majanga kumliko. Huu hata si mstari wa kutumiwa kabisa kwa mwanamke. Hufai kuutumia kwa mtu ambaye hata huyafahamu maisha yake. Naamini ukiutumia huu mstari hata kwa hirizi hutoboi.

1. Utumiaji wa mistari ya papo kwa hapo
Lazima mwanamume ana ile mistari ya papo kwa papo aliyoiweka kwa akili ambayo huitumia kila wakati akiwa na mwanamke. Kama wewe ni mtu wa aina hii itabidi uachane nayo kuitumia kwa demu mara ya kwanza. Hebu iangalie baadhi ya mistari yenyewe

Haya kazi kwako, kama wajiamini sahizi mshobokee yule mdada mrembo anayeishi kuleee...
Mistari 10 Ya Kutongoza Mwanamke Mara Ya Kwanza Unayofaa Kuiacha Mistari 10 Ya Kutongoza Mwanamke Mara Ya Kwanza Unayofaa Kuiacha Reviewed by Admin on Sunday, June 15, 2014 Rating: 5

1 comment:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.