Unordered List

Definition List

Kimye Wakataa Ofa Ya $11 Milioni Kuuza Picha Za Harusi, Kris Jenner Alaani Vikali

Kim Kardashian na Kanye West wanakumbwa na ushawishi wa kuuza picha zao za harusi kwa magazeti za udaku nchini Marekani.

Tukio la mwisho ni shawishi wa kupewa $11 milioni ili watoe picha hizo kulingana na madai ya New York Post. Kimye Walikataa.

Wajua alichosema mamake Kim Kris Jenner?


Kulingana na chanzo cha ndani ni kuwa Kris hana furaha kabisa na tukio hilo la wawili hao kukataa kiwango hicho kikubwa cha pesa(Kris anadai Kim ni kama ngombe wa maziwa aka cash cow)

Kris kikawaida anapata asilimia flani za pesa kutoka kwa watoto wake wote na hadi muda huu anapata faida kutoka filamu maarufu ya ngono ya Kim Kardashian.

Na sababu za Kimye kukataa ofa hio kubwa kulingana na chanzo kinadai kuwa wanataka kuzitoa pole pole kwa mashabiki wake kama vile picha za mtoto wa Beyonce Blue Ivy vilivyotoka.

Pia kuzitoa kwa upole kutaleta faida zaidi kuliko kuziachilia zote kwa mara moja.

Chanzo kinaendelea kueleza kuwa hawataki kurudia makosa ya awali ya ndoa za Kim ambapo baada ya muda mfupi kunazuka migogoro kati yao.

Yaonekana mzee mwenyewe Kanye West amekomaa kwa hii nyanga.

Cheki picha za harusi ya Kim Kardashian-Kanye West tulizonazo kutoka E!
Kimye Wakataa Ofa Ya $11 Milioni Kuuza Picha Za Harusi, Kris Jenner Alaani Vikali Kimye Wakataa Ofa Ya $11 Milioni Kuuza Picha Za Harusi, Kris Jenner Alaani Vikali Reviewed by Admin on Wednesday, June 18, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.