Unordered List

Definition List

Jinsi Ya Kumvutia Mwanamume Hadharani (Wanawake)


Wiki ya nyuma tuliweza kugusia kuhusu mistari ambayo wanaume hawafai kamwe kuitumia kwa siku ya kwanza wanapotongoza mwanamke, na sasa tunajeuza gurudumu kwa wanawake, Je, wajua mbinu ya kumvutia mwanamume yeyote hadharani?

Wanawake wengi bila kufundishwa wanaweza kudai kuwa wanaweza kuvutia mwanamume yeyote lakini ukweli ni kuwa wachache pekee ndio hufaulu.

Kama ungependa kumvutia mwanamume yeyote hadharani ama wataka kuongezea ujuzi wako basi zama nami.

Njia 8 Za Kumfanya Mwanamume Kukukimbilia Hadharani (Wanawake)

Tafuta sehemu mwafaka ya kukutana naye
Sehemu za hadhira waweza kukutana na mtu yeyote yule. Jukumu lako sasa ni kuchagua ile sehemu uitakayo wewe kukutana na mwanamume unayetamani. Sehemu za bar waweza kutana na mwanamume labda mlevi, sehemu za vibarazani waweza kupata mwanamume mvivu so itategemea na wewe mwenyeye ile sehemu wataka kukutana na mwanamume yeyote...labda hotelini yaweza kuwa sehemu murwa kwako.

Hakuna kitu kama 'na wale wengine'
Wakati ushamwona mwanamume sehemu flani, kitu ambacho anachofaa kukitia akilini mwako ni kuwa hakuna mtu mwingine isipokuwa MIMI. Wale madada wengine jifanye kana kwamba hawako kabisa na wala usiige mambo yao. Wewe jiweke unique. Jiweke tofauti kabisa. Unataka huyo mwanamume apende aina flani ya matendo, basi jitengeneze.

Eye contact aka mwangalie macho kwa macho kwa muda mrefu
Kumwangalia mwanamume kwa macho tutamfanya kukuona kuwa uko intrested na yeye. Ukimuangalia kwa macho zaidi halafu kumwonyesha tabasamu kutamfanya akukimbilie hapo kwa hapo. So nafasi kama hii usiiache.
Halafu kama umeona mwanamume aliyekuvutia waweza kumchezea gemu kiasi, haswa sehemu ambapo kuna watu wengi. Waweza kumwambia "Samahani nimepoteza kipuli changu na naomba usaidizi wako unisaidie kutafuta." Niamini huyo mwanamume ataomba hiko kipuli usikipate kamwe. Atataka nafasi ndefu ili aweze kuongea na wewe muda wote uwezekanao. Halafu jinsi utakavyotuma miondoko yako (kila mwanamke anaijua) kutamfanya asifikirie kwingine.

Valia kuvutia, lakini usivuke mipaka.
Mwanamke yeyote anaweza kumvutia mwanamume yeyote bora tu atumbie mbinu mwafaka. Bila kubabaikia umri, shepu, au urembo, mwanadada anaweza kuvalia nguo ambayo inaweza kumvutia yeyote. Pia uchunge usivuke mipaka kwa kuvalia nguo ndevu saana ana kuvalia nguo fupi sanaaa. Ile muhimu hapa ni kuvalia nguo ambayo unaweza kuivalia wakati wowote ule bila tatizo lakini bila kusahau ule mvuto wake.

Usijihusishe kwa kujiuza kwa uongo aka kuvalia kimitego
Wanawake wengi hapa ndipo kunapowachanganya sana. Wengi hudhania kuwa nguo za mitego huridhisha wanaume wote. La hasha, kuvalia kwa mitego huwa ni kuridhisha nuru ya macho pekee. Wanaume wengi hupenda sana kuona wanawake waliovalia kimitego lakini kuwaandama huwa ni tatizo kwani huona kama ni kinyume na maadili na tamaduni za kiafrika.

Valia lipstick ya rangi nyekundu
Rangi nyekundu huwavutia wanaume sana. Haijakulikana sababu ni nini lakini we fanya kujaribu kuvalia hio rangi tu utaona majibu yake.

Jiamini
Ili kuweza kuiteka hisia ya mwanamume lazima ujiamini kwa kila kitu. Wanaume hupenda wanawake aina hio. Wakati wa kuanzisha stori lazima ujihushishe pia. Waweza hata kuchukua mkondo wa stori na kuleta mada. Hii inaweza kumfanya asikusahau kwa urahisi hata kama kukutana kwenu hakukusongea zaidi ya maongezi.

Usiwe mtu wa pupa
Wanaume wanapenda wanawake wmbayo wako huru kuongea na wakati huo huo kuchagua. Usiwe mwanamke mwenye pupa ya kutaka mwanamume na kujionyesha kuwa una hamu, gemu yako icheze kwa wastani na hivyo basi itakuwa rahisi kwako kufanikiwa kumnasua.
Jinsi Ya Kumvutia Mwanamume Hadharani (Wanawake) Jinsi Ya Kumvutia Mwanamume Hadharani (Wanawake) Reviewed by Admin on Tuesday, June 24, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.