
Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kudai kuwa ujio wake mpya kwenye muziki atakuja pia na nyimbo za taarab, huku akimtaka Khadija Kopa ajiandae.
Akizungumza na Sporah Show hivi karibuni, Ray C amesema kwenye albam yake ambayo inakuja hivi karibuni kunamchanyiko wa nyimbo mbalimbali zikiwemo taarab na za kihindi.
“Nimefanya taarab kama mbili na zook, yani nimebadilishika kabisa, kuna kwaito , kuna bongoflava ,uwindi hindi kidogo, taarab nimeimba pia ,kwa hiyo Khadija Kopa ajiandae” Alisema Ray C.
Pia Ray C amedai kuwa aina ya muziki anaokuja nao kwa sasa hivi ni ule wa kuonyesha kipaji chake zaidi cha kuimba na siyo kucheza.
Albamu Mpya Ya Ray C Itajumlisha Taarab Na Kihindi
Reviewed by Admin
on
Monday, June 09, 2014
Rating:

No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano