Unordered List

Definition List

Hivi Lulu Michael Na Nando Ni Wapenzi!?


Stori: Musa Mateja na Mayasa Mariwata
Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe.

Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu. Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo.

“Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando.

Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyo huyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”
Hivi Lulu Michael Na Nando Ni Wapenzi!? Hivi Lulu Michael Na Nando Ni Wapenzi!? Reviewed by Admin on Monday, June 09, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.