Unordered List

Definition List

Justin Bieber Ajeuka Kuwa Mlokole, Afanyiwa Matambiko Kisiri


Kila siku inaposongea nyota ya mwimbaji huyu wa miaka 20 inazidi kufifia. Tukio la mwisho ni hivi majuzi ambapo video yake ilivuja akiwa anawatusi na kuwainjoy makabila mengine (racist jokes).

Hii ilikuwa pigo kuu kwa staa huyu wa nyimbo 'Confident' kiasi cha kumfanya kuingia kwa mtandao na kurusha video kadhaa za kuomba msamaha kuonyesha kuwa amesikitishwa na tukio hilo zima.

Kulingana na mtandao wa TMZ, staa huyu amechukua mkondo mwingine wa maisha...kumjeukia muumba wake.

Inasemekana kuwa Justin Bieber hivi karibuni alikuwa na Pastor Carl Lentz jijini New York City, ambapo alikuwa akifanyiwa mafundisho ya biblia na kuhudhuria makongamano kanisani.

Bieber aliweza kubaatizwa bafuni katika tubu ya rafiki yake (bathtub).

Kulingana na chanzo cha ndani, ilidaiwa kuwa Justin alitamani kubaatizwa kanisani kama kawaida lakini haikuwezekana kwa kuwa kila aendapo hufukuzwa na mapaparazi. Rafiki yake wa dhati alimtafutia sehemu ya kumfanyia matambiko hayo, ambapo ilikuwa ni kwa tubu.

Well, sasa itabidi tusimhukumu tena staa huyu.
Usikose stori zote za Justin Bieber zikiwemo skendo, nyimbo, video na zaidi
Justin Bieber Ajeuka Kuwa Mlokole, Afanyiwa Matambiko Kisiri Justin Bieber Ajeuka Kuwa Mlokole, Afanyiwa Matambiko Kisiri Reviewed by Admin on Monday, June 09, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.