Unordered List

Definition List

Ali Kiba; Diamond Platnumz Lazima Aje Kuniomba Msamaha Ili Issue Nzima Iishe

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongofleva afunguka tena kuhusiana na mambo mengi yanayosemwa na baadhi ya mashabiki kuhusu bifu yao na Diamond, hasa kwa kile kinachosemekana kuwa wawili hao ni paka na panya.

Ali Kiba akiwa anahojiwa na kituo kimoja cha redio alifunguka na kusema kuwa, yeye binafsi hana bifu na mtu yeyote hivi sasa, ni mambo tu yaliyowahi kutokea hapo nyuma ambayo hayakuwekwa sawa, alizidi kufunguka na kutoa fumbo kuhusiana na ishu yao na Diamond na kusemakuwa, Unaweza kulinganisha na siku unampa mwanafunzi mwenzako pepa lako kwenye mtihani ili akopi majibu, alafu mwisho wa siku anakuja kukwambia kuwa, pepa lenyewe halifai na kurudishiwa pepa hilo.

Ali Kiba alisema kuwa kwake yeye hana kinyongo na mtu, ila kwa lolote lilowahi kutokea Diamond mwenyewe ndio anayetakiwa kuja kumuomba msamaha Ali Kiba ndio mambo yaweze kuwa sawa.

Mbali na hayo Ali Kiba alifunguka na kusema kile kilichokuwa anakifanya wakati akiwa kimya bila kujibu chochote wakati uvumi na ugomvi huo ukizidi kuongelewa.

Alikiba alifunguka na kusema kuwa alikuwa bize kujifua kwa ujio wake mpya, hasa kwa Project zake anazokuja nazo upya hivi sasa.

Mbali na kuongelea Ugomvi wao huo baina yake na Diamond, Ali Kiba alisema kuwa hivi sasa ndio kaja rasmi kuwashika, kaja kuchukua ufalme wake baada ya kutawaliwa kwa muda mrefu sasa kwenye tasnia hii ya Bongo Fleva.

Hii sentensi ilikuja na ujio wake mpya wa KibaSquare, kama kundi flani hivi linalojumuisha yeye mwenyewe Ali Kiba na Mdogo mtu, ambao wameweza ku-drop hit track yao iitwayo Pitambele, inayotarajia kufanya vizuri sana kwenye ulimwengu wa muziki.

Chanzo na vibe
Ali Kiba; Diamond Platnumz Lazima Aje Kuniomba Msamaha Ili Issue Nzima Iishe Ali Kiba; Diamond Platnumz Lazima Aje Kuniomba Msamaha Ili Issue Nzima Iishe Reviewed by Admin on Friday, June 20, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.