Unordered List

Definition List

Diamond Platinumz Ampangia Makubwa Wema Sepetu


Kama ulikuwa unadhani kuwa Diamond alikuwa amemsahau baby wake katika suala zima la kutoka ki-international zaidi, subiri sana.

Diamond ameweka wazi nia yake ya kumtoa ki-movie Wema Sepetu na tayari ameshaweka mambo sawa kwa wadau wa sekta ya filamu huko nchini Ghana.

Diamond alizidi kufunguka kuhusiana na plan yake na kusema kuwa ameshaongea na mdau fulani hivi aliyeko huko Ghana aliyetajwa kwa jina moja la Frank, ambaye ndiye anayeandaa tuzo nyingi huko nchini Ghana na ana-connection za kila kona kwenye sekta za filamu, na kumuelezea kuhusiana na kazi za mpenzi wake huyo, kama njia ya kumpa shavu ili aweze kufanya mambo kwa next level zaidi.

Mbali na mdau huyo pia Diamond amefunguka na kusema kuwa ameshaongea na baadhi ya wacheza filamu maarufu kama akina Van Vicker na wengine kibao wanaoshikilia masoko makubwa ya filamu nchini Ghana na Nigeria na tayari process za kufanya mipango zinaendelea na soon kutarajia kazi za Wema zikienda kimataifa zaidi kama ilivyo kwake Diamond Platnumz hivi sasa.
Diamond Platinumz Ampangia Makubwa Wema Sepetu Diamond Platinumz Ampangia Makubwa Wema Sepetu Reviewed by Admin on Friday, June 27, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.