Unordered List

Definition List

Nando Afunguka Kuwa Hana Mahusiano Na Lulu, Lakini Amemvutia


Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa (the chase) 2013, Amir Nando ameweka wazi kuwa hajawai kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanadada wa filamu, Elizabeth Micheal aka Lulu, lakini anakubali sana.

Akizungumza na Global Tv ,Nando amezungumzia pia mipango yake ya kufanya filamu na mwanadada huyo wa filamu. “Lulu nishaonana nae, mara mbili mara tatu lakini sina uhusiano nae na sijawai kuwa na uhusiano nae, ila namkubali sana, mwanamke unajua mzuri, shepu, mwonekano wake, michezo yake, tunaonana tu ile oya niaje mara mbili maratatu.

Na proposal mimi, akitaka tukae chini tutengeneze movie, hicho ndicho nachotakanifanye, akikubali tutafanya, lakini Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake” Alisema Nando
Nando Afunguka Kuwa Hana Mahusiano Na Lulu, Lakini Amemvutia Nando Afunguka Kuwa Hana Mahusiano Na Lulu, Lakini Amemvutia Reviewed by Admin on Monday, June 09, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.