Unordered List

Definition List

Msanii Wa Kenya Kutoa Video Akiwa Nusu Uchi

Hii mitindo mipya ya wasanii wa kike kutoa video wakiwa uchi sijui inaelekea wapi...tangu mwaka jana hadi sahizi kumekuwa na misururu ya video nyingi zikiwahusisha mastaa akina dada kutoa video za uchi bila wasiwasi.

Siwezi kujua chanzo chake kimeanzia wapi, na wala siwezi kusema video za Miley Cyrus akiwa uchi ndizo chanzo kikuu, tabia hii inaonekana imetoka mbali.

Na tatizo hili limeingia hadi Afrika kwa ujumla. Wanadada kadhaa wameamua kujitundika na video za uchi kama njia ya umaarufu...hivi karibuni ni ule uandalizi wa video ya uchi ya msanii wa Injili nchini Nigeria Maheeda(ni video ya nyimbo ya injili nikieleza kwa urahisi), tunafikia wapi?!?
Chess katika snapshot ya video yake mpya
Sasa nchini Kenya mwanadada Chess Nthusi ameamua kuwapima imani mashabiki wake kwa ujumla, kwa kutoa video akiwaonyesha matamanio ya kimwili. Bado video yenyewe iko jikoni ikiandali.

Huyu Chess Nthusi ndiye nani?

Mmmmh...ni msanii ambaye ashawahi kutoa kolabo na Prezzo katika nyimbo ya 'Celebration For Life' na pia kutoa kolabo na Kaligraph 'Hold You Down'....na video anayopania kutoa inaitwa 'Am In Love'.

ok! hebu tumuache ajaribu bahati yake, nani anaweza kujua kama atapata umaarufu zaidi kama vile video ya ngono ya Kim Kardashian ilivyomfanya staa,,
Msanii Wa Kenya Kutoa Video Akiwa Nusu Uchi Msanii Wa Kenya Kutoa Video Akiwa Nusu Uchi Reviewed by Admin on Thursday, March 13, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.