Unordered List

Definition List

Mamake Wema Sepetu Apoteza Cheti Cha Mazishi Cha Marehemu Mumewe

NI balaa ni nini? Mariam Athuman Sepetu ambaye ni mama mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ametinga katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kutoa taarifa ya kupotelewa hati ya uthibitisho ya kifo cha mume wake, marehemu Isaac Sepetu.
.
Vyanzo  kutoka ndani ya jeshi la polisi vinasema kwamba, mama Wema alifika kituoni hapo Machi 19, mwaka huu na kutoa taarifa hiyo yenye kumbukumbu KJN/RB/2499/2014 na alihofu kuwa huenda hati hiyo iliibwa na wajanja wenye nia mbaya.

Cheki Picha Za Mazishi Ya Babake Wema Sepetu

Ilidaiwa kuwa siku ya tukio saa nne usiku, mama huyo aliitafuta hati hiyo ili kesho yake akafungue madai ya mirathi ya mumewe lakini hakuiona mahali alipoiweka jambo lililomfanya aende polisi kuwajulisha.
Hati hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha kipolisi  hati hiyo ilitolewa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar, Oktoba 27, mwaka jana.
http://api.ning.com/files/72Jod1iYAGGHHQ1TU41LY3dmk7ymPWECvwdUWdZbBnlEbLiZs2CWBqAqLu7-KisoFWFIgbcHv3IXuOzEPPMk9KzZjCdPlQMS/22222.jpg
Mamake Wema Sepetu, Mariam Athman Sepetu

Jumapili iliyopita, Uwazi lilimtafuta mama huyo ili kujua kama yeye ndiye aliyefikisha taarifa hizo polisi.
“Nililazimika kwenda huko kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee na sikuweza kujua kama aliyeichukua alikuwa na nia gani, lakini hata hivyo baada ya siku kadhaa kupita tangu nitoe taarifa niliitafuta tena nikakuta imerudishwa,” alisema mama Wema.
Mamake Wema Sepetu Apoteza Cheti Cha Mazishi Cha Marehemu Mumewe Mamake Wema Sepetu Apoteza Cheti Cha Mazishi Cha Marehemu Mumewe Reviewed by Admin on Tuesday, March 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.