Zile speculation kuwa huenda star mpya wa Hollywood Lupita Nyong’o ana uhusiano wa siri na mwigizaji mwenzake Jared Leto zimezikwa na speculation mpya kuwa huenda rapper na mwimbaji wa Somalia aitwaye K’naan ndiye mpenzi wa Lupita.
Picha mbalimbali zilizosambaa siku moja baada ya Tuzo za Oscar zikiwaonesha Lupita na rapper K’naan mwenye asili ya Somalia, wakiwa katika pozi zinazoashiria ukaribu mkubwa ndio zimezua speculation hizo.Keinan Abdi Warsame a.k.a K’naan ambaye amewahi kuhit na single yake ‘Waving Flag’ mwaka 2010, walionekana wakiwa pamoja siku ya Jumatatu wakati Lupita akitoka kufanya mahojiano na Live.
Ripoti zinasema kuwa K’naan pia alikuwepo katika matukio ya awali kabla ya siku ya Tuzo za Oscar kumpa support Lupita, na Lupita amekuwa akisema jinsi anayopenda muziki wake kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, na mwezi uliopita (February 27) alihudhuria show yake Hotel Café, huko Los Angeles ambayo pia alimsaidia kumfanyia promo.
Lupita Nyong'o Na K'naan Wanamahusiano Kiuchumba!!!
Reviewed by Admin
on
Saturday, March 08, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano