Unordered List

Definition List

Diamond Platinumz Apooza Shughuli Zote Za Coco Beach Ili Kufanya Shoo Ajab (PICHA)

Imekuwa siku hizi kila mahali utasikia jina la Diamond Platinumz likiingizwa kwa mijala tofauti.

Na mijadala yenyewe si kwa sababu anakumbwa na kashfa wala nini bali ni vile msanii huyu anafananishwa kama moto unaoteketea kwa nyasi kavu...anaiteka hisia za Afrika nzima. Baadhi ya matukio ya kuashiria staa huyu anawika ni pale aliposhika #1 katika kituo cha runinga cha TRACE TV chenye makaazi nchini Afrika Kusini.

Kutia kidonda msumari wa moto ni kuwa kuna baadhi za blog na mitandao zinazodai kuwa Diamond Platinumz anagombaniwa kama maji ya jangwani na mastaa watajika wa Nigeria na Ghana. Kiufupi nasema staa huyu ni mtu anayechuna matawi ya juu.

Tukirudi nyumbani ni kuwa staa huyu ameweza kulemaza shughli zote pale Coco Beach wikendi ya jana ili kufanya shoo ya kuwaburudisha wote waliohudhuria.

Cheki baadhi ya tukio lote zima lililojiri wikendi.

clip_image001Diamond Platnumz akiwa anapanda jukwaani katika show iliyofanyika Jana Pale coco Beachclip_image001[5]Diamond Platnumz akiwasiri katika Fukwe ya COCO beach kwa ajili ya Show yake akiwa na baunsa wake kwa ajili ya Usalamaclip_image001[7]Ma Dj wakiweka mambo sawa Kwa ajili ya Show hiyo iliyofanyika katika fukwe ya Coco Beach Mjini Dar es salaamclip_image001[9]Kama ilivyo kawaida yake Watu walifurika Katika Viwanja hivyo kwa ajili ya Kushuhudia Show ya Mkali huyo wa Bongo Fleva akitoa burudani ya Nguvuclip_image001[11]Yeah ni Mambo ya Ku ringa ringa Hadi wanadaaaaaata……..clip_image001[13]
clip_image001[15]Wingi wa watu uipelekea kutokea Msukumano wa hapa na pale na Kupelekea Hali hii kutokea mara kadhaa…..clip_image001[17]Diamond akiwapa mashabiki kile alichotaraji kuwapatia katika Show yake hiyo… Ilikuwa ni Burudani ya Aina yake.clip_image001[19]Team Wasafi wakiwa kazini

Picha kwa hisani ya BongoClan
Diamond Platinumz Apooza Shughuli Zote Za Coco Beach Ili Kufanya Shoo Ajab (PICHA) Diamond Platinumz Apooza Shughuli Zote Za Coco Beach Ili Kufanya Shoo Ajab (PICHA) Reviewed by Admin on Monday, March 24, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.