Unordered List

Definition List

Kozi Ya 'The Sociology of Miley Cyrus' Kufunzwa Katika Chuo!

Wakati wa msimu wa kiangazi 'summer' nchini Marekani wanafunzi wengi huchukia masomo.

Lakini college ya Skidmore inapaniwa kusajili wanafunzi wengi mwaka huu, shukrani zote zikimuendea profesa msaidizi Carolyn Chernoff, ambaye amekuja na kozi kali ya kufundisha wanafunzi wa chuo hicho.

Kozi yenyewe inajulikana kama 'The Sociology of Miley Cyrus'



Kama iliyoelezwa katika picha hapo juu kozi hii usitarajie kama itafunza watu kudengua makalio a.k.a Twerking wala usitumainie kama kutakuwa na mafunzo ya kutemea mate hadhira yako.

Bali kozi hii itaeleza na kujikita kwa mwanadada huyu ambaye alianza maisha yake tangu alipokuwa Malkia wa Disney. Pia itagusia maisha ya wasanii kama vile Justin Timberlake, Britney Spears, na Christina Aguilera.

Mambo mengine yatakayofunzwa ndani ya kozi hii ni ikiwemo.
  • Utofauti wa ujinsia na mabadiliko ya utoto
  • Njia kadhaa ambazo watu hupitia hadi kubalehe
  • Matumizi ya utamaduni, kabila nk
  • Ujinsia tofauti wa wanawake
Unaionaje kozi kama hii, waweza kuichukua?
Kozi Ya 'The Sociology of Miley Cyrus' Kufunzwa Katika Chuo! Kozi Ya 'The Sociology of Miley Cyrus' Kufunzwa Katika Chuo! Reviewed by Admin on Friday, March 28, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.