Unordered List

Definition List

Ushoga Kuangamizwa Kenya; Mbunge Aongoza Sheria Kali

Nairobi. Mbunge Irungu Kang’ata anaongoza juhudi za kundi lililoundwa la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini  Kenya. Sheria zilizopo zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela.

Huenda ikawa nchi inayofuata kwenye utata unaohusiana na haki za wapenzi wa jinsia moja, huku wabunge wakipanga kuwasilisha muswada bungeni kushinikiza Serikali kufanya juhudi zaidi kutekeleza sheria zilizomoza kupiga marufuku ushoga.

Kwa upande wao wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema shinikizo limeongezeka tangu nchi jirani ya Uganda ilipopitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi uliopita.

Irungu Kang’ata ambaye ni mbunge kwa mara ya kwanza anaongoza juhudi za kundi lililoundwa majuzi la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya. Katika kampeni za wazi kabisa, mbunge huyo ameomba chama tawala kuelezea Serikali inachukua hatua gani kutekeleza sheria zilizopo dhidi ya mashoga.

Sheria zilizopo nchini  Kenya zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo  cha miaka 14 jela.

Kundi hilo linalopinga wapenzi wa jinsia moja  liliundwa majuzi wakati Rais wa nchi jirani ya Uganda Yoweri Museveni alipotia saini sheria dhidi ya wapenzi wajinsia moja mwezi Februari, licha ya shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi asitie saini.
Ushoga Kuangamizwa Kenya; Mbunge Aongoza Sheria Kali Ushoga Kuangamizwa Kenya; Mbunge Aongoza Sheria Kali Reviewed by Admin on Saturday, March 08, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.