Unordered List

Definition List

Chris Brown Ajiskia Kama Mnyama Aliye Kizimbani: Anachukia Maisha Ya Jela

Chris Brown anatamani asingelikuwa jela.

Baada ya kufukuzwa kutoka rehab kwa mara ya pili chini ya miezi kadhaa kwa kukiuka masharti 3, staa huyu amehukumiwa kutiwa jela kwa mwezi mzima.

Huku akiwa kizimbani kwa masaa 23 akiwa pekeyake, mwanamziki huyu ameshindwa kustahimili kabisa. Chanzo kutoka TMZ kiliongea.





Chris Brown anajiskia kama mnyama aliyetiwa kizimbani, chanzo kilidai huku Chris akishuhudia kuwa tukio hili ndilo baya zaidi kutokea kwake tangu azaliwe.


Nje ya mada pia Rihanna ashasema kuwa kupigwa na Chris Brown usoni hadi kutokwa damu ilikuwa ni tukio baya kabisa kuwahi kutokea maishani mwake.

So Chris Brown anafanya nini muda wote akiwa kizimbani peke yake?

Chanzo kinadai kuwa Chris amekuwa mbunifu kwa kuandika nyimbo mpya na kufanya mazoezi kujenga mwili. Pia Chris anadai kuwapigia marafiki zake simu kuwa maisha ya jela yamemtamausha na hatodhubutu tena kufanya makosa ya kijinga

Haijulikani hatima ya staa huyu itakuwaje, labda anaweza kuhukumiwa kifungo kwa makosa yake ama kuachiliwa huyu.





Chris Brown Ajiskia Kama Mnyama Aliye Kizimbani: Anachukia Maisha Ya Jela Chris Brown Ajiskia Kama Mnyama Aliye Kizimbani: Anachukia Maisha Ya Jela Reviewed by Admin on Sunday, March 23, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.