Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu hiyo ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako Wema na Aunt wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao mpya ya Familia.
Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa sasa wapo ‘kloz’ kiasi cha watu kuwa na maswali vipi kuhusu Kajala Masanja, walipiga picha hizo wakidhamiria kuzifuta baada ya kujiona lakini lililotokea si akili zao, picha hizo zikanaswa na paparazi wetu.
Juzi, Amani liliwatafuta kwa njia ya simu wawili hao na kuwauliza nini kiliwatia nguvu hadi kupiga picha hizo ambapo Wema Sepetu anaonekana akibusu sehemu ya paji la uso la Aunt huku naye akiwa amelegeza macho kusikilizia.
Wema: “Unajua huyu Aunt ni mtu ambaye tumezoeana kupita kiasi, tunapomaliza kufanya kazi, tunaanza utani. Halafu kwetu mbona mabusu ni ishu ya kawaida sana!”
Habari za ndani zinasema, baadhi ya ndugu wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’ huyo kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya mume wake licha ya kutotoa tamko lolote.
Mbali na Dimonte, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walimtaka Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukaa chini na kufikiri upya kuhusu uamuzi wake wa kumuoa Wema. Wengi wanaamini si sahihi kwake kwa vile haonekani ‘kutulia’ licha ya kwamba wote ‘hawajatulia’
Wema Sepetu Na Aunt Ezekiel Ni Wasagaji?
Reviewed by Admin
on
Thursday, March 27, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano