Unordered List

Definition List

Lady Gaga Atetea Tukio Zima La Kutapikiwa Katika Jukwaa

Lady Gaga si mtu wa kuona haya wakati wa kutetea matukio anayofanya.

Mwanadada huyu anayevuma kwa albamu yake mpya ya Artpop alikuwa anahojiwa kuhusu tukio zima ambalo lilifanyika wiki iliopita kuhusu Lady Gaga kutemewa matapishi wakati wa kufanya shoo ya nyimbo 'Swine'.

So Lady Gaga alikuwa na yapi ya kusema?

"Hatukushangazwa na tukio hili kwani mimi na Millie tulijua kuwa kuna wengine wangependa shoo yetu na wengine pia hawangependa tukio hili."

Mbona sasa muliamua kufanya jambo hili?

"Tunaamini usanii zaidi na nguvu za sanaa zetu. Mimi namsapoti kwa kila jambo [Millie] na albamu yangu ya ARTPOP inaunganisha sanaa na nyimbo kwa pamoja ili kuleta upinzani mkubwa. Kwetu sisi tukio hilo lote zima lilikuwa sanaa katika tajriba ya juu."

Cheki mahojiano yote ya Lady Gaga na kituo cha Today:



Lady Gaga pia alidai kuwa tukio hilo lote halikuwa eti kuzua tetesi bali alifanya hivyo kuwaburudisha mashabiki wake wote
Lady Gaga Atetea Tukio Zima La Kutapikiwa Katika Jukwaa Lady Gaga Atetea Tukio Zima La Kutapikiwa Katika Jukwaa Reviewed by Admin on Sunday, March 23, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.