Unordered List

Definition List

Ray C Atukumbisha Enzi Zake Za Kiza

Stori iliyozuka wiki iliyopita na kuleta mijadala mikali ni kuwa Ray C anatafuta mbinu za kumtega Diamond Platinumz kutoka kwa Wema Sepetu....kiufupi Ray C anamtamani Diamond Platinumz.

Tukiachana na mambo ya kugombea waume za watu, Ray C ameturudisha nyuma kimiaka...kutukumbuka wakati alivyokuwa akiteseka na madawa ya kulevya.

Katika mtandao wake wa Instagram mwanadada huyu alikuwa na ujumbe muhimu kwa wote wanaotumia madawa ya kulevya na wale ambao wanatamani kujihusisha. Mwanadada huyu anakuonya kuhusu maovu ya dawa hizi.

Ray C miezi tu ya juzi aliweza kutimiza mwaka mmoja bila kutumia mihadarati na kila siku anazidi kuwa mwanamke mwenye afya.

Katika Instagram aliweza kuweka picha na maneno:
“STOP USING DRUGS PEOPLE…..DRUGS KILL….MLIOKO TOKENI JAMANI!!!THANK YOU GOD…….FREE AT LAST.”

Ray C Atukumbisha Enzi Zake Za Kiza Ray C Atukumbisha Enzi Zake Za Kiza Reviewed by Admin on Tuesday, March 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.