Unordered List

Definition List

Laana!! Kanisa Lakataza Waumini Wake Kuvalia Chupi Na Sidiria Wakati Wa Ibada


Hivi baada ya kanisa moja nchini Marekani kuruhusu waumini wake kuabudu wakiwa uchi mnyama, sasa wimbi hilo limeanza kushika kasi katika baadhi ya makanisa Afrika Masharika haswa jijini Nairobi.

Makanisa kadhaa jijini Nairobi yameanza kufuata mitindo isiyo ya kawaida huku kanisa moja (Mavuno Church) linajivunia kuweka mabango ya picha za ngono ili kuwavutia vijana kwenda kufanya ibada kwayo.
Pia hivi karibuni pasta alinaswa katika fumanizi na wanahabari katika gesti kisa na maana eti alikuwa akimbariki mwanakondoo.

Vitendo vingi vya uovu vinaendelea kujitokeza nchini Kenya na Afrika nzima kiujumla huku wengine wakienda mipaka ya kumpima Mungu imani.

Kikawaida kila kanisa huwa na sheria fulani ambazo hukisiwa kufuatwa na waumini na wahubiri kiujumla, lakini cha kushangaza ni kanisa moja Nairobi, kitongoji cha Dandora kimeshangaza wengi.

Kutoruhusu wanawake kuvalia chupi wala sidiria!

Kulingana na wadadisi kutoka mtandao wa Nairobi Exposed, kanisa moja kitongoji cha Dandora limeamua kufuata sheria zao wenyewe, kutoruhusu waumini wa kike kuvalia chochote ndani kujistiri. Kulingana na mwandani wa kanisa hilo la Lord's Propeller Redemption Church, inasemekana wakuu wa kanisa hilo walifanya kura ya siri ili kuhakikisha mswada huo unapitishwa.

Kulingana na pasta anaongoza kondoo hao inadaiwa kuwa anamini 'kuvalia nguo za ndani ni kitu ambacho si cha kiungu na ameonya yeyote atakayekiuka sheria hio basi atakabilana na sheria kali kutoka katika kanisa hilo.

"Tumeonywa na kuambiwa kuwa kama tunaenda kanisani tushauri wake zetu na watoto wetu wa kike wasivalie chochote ndani." mwandani mmoja aliongea na mtandao wa NE

Cha kushangaza ni kuwa tangu sheria ipitishwe katika kanisa hilo, waumini wamekuwa wakifuata bila tatizo lolote.

Twafikia wapi kama jamii?

Soma: Pasta Anayehubiri Na Nyoka Shingoni
          Mhubiri Agusa Nyeti Za Mwanamke Wakati Wa Maombi
Laana!! Kanisa Lakataza Waumini Wake Kuvalia Chupi Na Sidiria Wakati Wa Ibada Laana!! Kanisa Lakataza Waumini Wake Kuvalia Chupi Na Sidiria Wakati Wa Ibada Reviewed by Admin on Monday, March 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.