Unordered List

Definition List

Pastor Afa Maji Baada Ya Kujaribu Kutembea Juu Ya Maji Kama Yesu

NIGERIA. Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumoni baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.


Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi.

Mfuasi wa Yesu, Peter alijaribu kutembea juu ya maji kama vile Yesu alivyofanya lakini hakutoboa, alisaidiwa kuzama maji. Sasa miaka zaidi ya 2000 baadae, pastor huyu wa Nigeria alijaribu kumuiga Yesu lakini hakufaulu na majibu yake ni kuwa alipoteza maisha yake.

Ama pastor huyo aliingiwa na imani kuwa anaweza kutembea juu ya maji kama vile wale 'magician' wa vipindi vya runinga wanavyofanya.
Pastor Afa Maji Baada Ya Kujaribu Kutembea Juu Ya Maji Kama Yesu Pastor Afa Maji Baada Ya Kujaribu Kutembea Juu Ya Maji Kama Yesu Reviewed by Admin on Friday, January 03, 2014 Rating: 5

1 comment:

  1. Amejaribu kupima imani ya mwenyezimungu huyo

    ReplyDelete

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.