Unordered List

Definition List

BABA KANUMBA AFUNGUKA, NI KWELI ANAMCHUKIA LULU MICHAEL?!?

Lulu Michael
Baba Kanumba
Tarehe 7 mwezi huu Lulu Michael alikuwa mwenye furaha wakati alipokuwa akisherehekea kuzaliwa kwa mama Kanumba. Ilikuwa furaha kuu huku akiweka picha zake na za mamake Kanumba kwa Instagram

Lakini je, babake marehemu Kanumba ana yapi kuhusu haya yote, je anamchukia shetani mwenyewe Lulu Michael.

Kwa mitandao kumekuwa na mijadala na tetesi kuwa babake Kanumba anamchukia Lulu lakini chanzo kinachoaminika kiliweza kubainisha kati ya mbivu na mbichi.

Alipoulizwa, baba Kanumba alikuwa na haya ya kusema:
‘Mimi Lulu sijamchukia… tangu zamani wananiuliza nasema sina ugomvi na Lulu kwa sababu walikua watu wawili, walikua wapenzi wawili….. hatuwezi kuingilia watu walikua chumbani utajuaje nani kamuanza mwenzake? alafu wakiniingiza mimi kwamba namchukia Lulu.. hata siku moja sijawahi kumzungumzia, hao watu walipakazia na ni waongo…. siwezi kumchukia Lulu wala kumjadili’

Kwa hayo maneno inadhihirisha kuwa hakuna ugomvi wowote kati ya wawili hao.
BABA KANUMBA AFUNGUKA, NI KWELI ANAMCHUKIA LULU MICHAEL?!? BABA KANUMBA AFUNGUKA, NI KWELI ANAMCHUKIA LULU MICHAEL?!? Reviewed by Admin on Saturday, January 11, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.