Unordered List

Definition List

NIVA, Msanii Wa Bongo Movie Ala Kichapo Kutoka Kwa Demu Wake

Zuberi Mohamed

Mcheza  filamu Zuberi Mohamed‘Niva’ juzi alijikuta akipata fedheha baada ya kupigana na mwanamke anayesemekana kuwa kama ni mpenzi wake, sakata hilo la aibu lilitokea katika Hotel ya Ndeka iliyopo maeneo ya Magomeni, tukio hilo lilitokea mida ya saa tano usiku. Walioshuhudia tukio hilo amesema kuwa Niva alikuwa kapanga katika Hoteli hiyo na baadae alikuja na binti huyo na kuagiza chakula na kupelekewa chumbani huko ambako ugomvi ulitokea na kusababisha vurugu zilimfanya Niva kutoka nduki.

Kufuatia ugomvi huo uliotokea ghorofa ya tano chumba namba 5, msanii huyo alitoka nduki akiwa na nguo ya ndani tu na kukimbia hadi chini na kutoweka jambo lilofanya wahudumu kuingia katika chumba hicho na kushuhudia uharibifu uliofanywa na wapenzi hao, huku kuta za chumba hicho zikiwa zimetapakaa kwa uchafu wa vyakula.

Msanii hiyo katika tukio hilo amepoteza vito vya thamani kama vile saa, mkufu, simu na vitu vinginevyo, hadi habari hizi zisizo na shaka zinatufikia msanii huyo alikuwa hapatikani katika simu yake ya mkononi, ili aweke wazi kilichopilekea ghafla na mpenzi wake kugeuzaa Hoteli ulingo wa masumbwi.
NIVA, Msanii Wa Bongo Movie Ala Kichapo Kutoka Kwa Demu Wake NIVA, Msanii Wa Bongo Movie Ala Kichapo Kutoka Kwa Demu Wake Reviewed by Admin on Thursday, January 23, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.