Unordered List

Definition List

NISHA Afunguka Baada Ya Skendo Ya Kuavya Mimba


bkuHABARI
Wakumbuka ile skendo iliyomkumba Nisha kuwa anaugua baada ya kuavya mimba? Sasa amejitokeza wazi baada kuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu hili jambo.

Nisha aka Salma Jabu amefunguka akidai kuwa maendeleo yake katika filamu yamemtengenezea maadui.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nisha alisema maadui hao wamefikia hatua ya kumzushia kuwa ametoa mimba au ‘ame-flush’ wakati anaumwa na kichwa.

Alisema amebaini kuwa ana maadui wengi ambao hawapendi kuona anavyoendelea na ndio maana wamekuwa wakimzushia maneno yanayomchafua katika jamii.
“Huku Bongo Movie hatari sana, hata ukiwa na rafiki yako kuwa makini naye kwani ipo siku atakuuza na kukupoteza, mimi sifuatilii mambo ya mtu mwingine zaidi ya biashara zangu na kazi yangu tu,’’ alisema.

“Bongo Movie kuna watu wanaotaka kila siku wajue Nisha kafanya nini ili wakuseme vibaya, kuwa na maendeleo ni kutengeneza maadui nahisi kuwa na maadui pembeni yangu,” aliongeza Nisha.
Nisha ambaye hivi karibuni alikuwa mgonjwa, alitoa kauli hiyo baada ya kuripotiwa maradhi yaliyokuwa yakimsibu chanzo chake ni mimba aliyoitoa.

Hata hivyo Nisha aliwashangaa waliomzushia hilo na kufafanua kuwa alikuwa anaumwa kichwa na kama ingekuwa ametoa mimba angekuwa anaumwa tumbo.
NISHA Afunguka Baada Ya Skendo Ya Kuavya Mimba NISHA Afunguka Baada Ya Skendo Ya Kuavya Mimba Reviewed by Admin on Saturday, January 18, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.