Unordered List

Definition List

Kim Kardashian Apeleka Ripoti Kwa Polisi: Kuna Mtu Amemtishia Kumuua

Siku ya Jumanne ilikuwa kizaa zaa kwa Kim na Kanye wakati walipoenda kutembelea daktari ambae aliagana kukutana na Kim kwa check up yake ya kawaida. Walikumbana na jamaa ambaye alikuwa anawachukia.

Kulingana na habari, insemekana Kim Kardashian alikuwa katika hospitali ya Beverly Hills kabla jamaa huyu kuanza kuwatusi mapaparazi kabla kumjeukia Kim mwenyewe.

Gazeti la TMZ linadai kuwa jamaa huyo mwenye miaka 19 alimtishia Kim na kumwambia kuwa atamuua. "I will kill you slut" Jamaa huyo mwenye asili ya kiafrika alimtishia Kim Kardashian. Kim sasa ameenda polisi kuweka madai kuwa maisha yake yamo hatarini.

Pia wakati wa rapsha hio, Kanye West alitojitokeza kutoka chumba cha kusubiri kabla kumshambulia jamaa huyo .

Kanye  tayari ana kesi inayomngojea kotini kwa kumpiga paparazi na wakili anayemtetea Kanye anadai kuwa kesi ya Kanye ni tofauti na inafaa kutupiliwa mbali, jambo ambalo jaji mkuu bado hajakubaliana nalo.

Kanye kujaribu kumpiga kijana huyu kutamtia hatarini, labda ndio maana Kim amewasilisha malalamishi kuwa maisha yake yamo hatarini.



Kim Kardashian and Kanye West: Behind the Attack
Kim Kardashian Apeleka Ripoti Kwa Polisi: Kuna Mtu Amemtishia Kumuua Kim Kardashian Apeleka Ripoti Kwa Polisi: Kuna Mtu Amemtishia Kumuua Reviewed by Admin on Thursday, January 16, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.