Unordered List

Definition List

Kipato Cha Diamond Platinumz, Je Wajua Analipwa Ngapi Kufanya Shoo Moja?!?

Bila shaka msanii huyu anayetamba sahizi kwa nyimbo yake mpya ya My Number One remix ni staa wa kulengwa kwa manati.

Diamond Platinumz kwa sasa yupo na anazidi kuendelea kuwepo kila uchao. Staa huyu anayegonga vichwa vya habari kila siku amedhihirisha kuwa ameweza kuistadi tasnia ya mziki na kuijua nje na ndani jinsi ya kufanikisha mziki na umaarufu wake.

Platinumz ni msanii anayemiliki pesa nyingi, dhihirisho lake moja ni thamani ya video yake mpya ya My Number One Remix na nyingine jumba analolijenga sahizi na pia bling zake za dhahabu.

Lakini je msanii huyu pesa zake huzitoa wapi?

Usanii hulipa bora tu uwe mjanja. Kulingana na mwanahabari mwenye uhusiano wa karibu na mastaa wengi, Willy M Tuva, mwendeshaji wa kipindi cha muziki wa kizazi kipya nchini Kenya amebainisha kuwa Diamond ni mfano wa matawi ya juu.

Tuva alibainisha kuwa kama unataka kumkodisha Diamond aje akufanyie shoo usiku mmoja lazima uwe na dola $20,000. Diamond atagharamia mengineyo kama dansa, uchukuzi nk.

Hizi ukizijeuza pesa za kibongo ni takriban milioni 32,000,000 usiku mmoja pekee...kiufupi Diamond ameonyesha kuwa ataendelea kuwakandamiza wasanii wenzake kwa upande wa mashabiki, umaarufu na.....kimkwanja.

Nani alisema mziki hauna faida?

Kipato Cha Diamond Platinumz, Je Wajua Analipwa Ngapi Kufanya Shoo Moja?!? Kipato Cha Diamond Platinumz, Je Wajua Analipwa Ngapi Kufanya Shoo Moja?!? Reviewed by Admin on Friday, January 17, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.