Unordered List

Definition List

Tukio Lililojiri Wakati Ferooz Alipotiwa Pingu Na Polisi Baada Ya Kunaswa Akivuta Bangi(PICHA)

Staa aliyesifika sana enzi zake kwa nyimbo silizoibua hisia kwa masikilizaji Ferooz alinaswa na polisi baada mdaku mmoja kuudhiwa na viendo vyake vya kuvuta bangi hadharani bila mipangilio.

Akiwa na Kundi la Daz Nundaz, Ferooz Mrisho, hivi juzi alikamatwa na polisi na kutupwa lupango katika Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kulingana na wakaazi waliokuwa wakiishi sehemu ambazo staa huyo alinaswa walikuwa wakilalamika kwa matendo ya kuudhi yaliyokuwa yakifanywa na staa huyo wa zamani.

“Hapana tumechoka na tabia zao, kila ukipita hapa unakula ‘marashi’ ya bangi tu, vilevile sisi tuna vijana wa rika lao, hawa vijana wanaopita hapa wanasoma,  tunaogopa sana wasije wakajiunga na wao hapa kula ganja,” mama mmoja aliongea kwa uchungu wakati wa tukio lote hilo.


Cheki matukio yaliyojiri kwa picha hapo chini:

akiwa mikononi mwa polisi
akishukishwa kutoka kwa gari
akiwa ametiwa pingu na mwenzake
Tukio Lililojiri Wakati Ferooz Alipotiwa Pingu Na Polisi Baada Ya Kunaswa Akivuta Bangi(PICHA) Tukio Lililojiri Wakati Ferooz Alipotiwa Pingu Na Polisi Baada Ya Kunaswa Akivuta Bangi(PICHA) Reviewed by Admin on Thursday, January 16, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.