Unordered List

Definition List

Babu Wa Loliondo...Maisha Ya 'Kitajiri' Ya Sasa

Babu wa Loliondo a.k.a kikombe cha uzima aliweza kutikisha karibu Afrika nzima kwa madai ya kuwa yeye anaweza kupona ugonjwa wowote kupitia dozi moja ya dawa wa maji pekee.

Wengi walitekwa na jambo hili na kufanya matajiri, maskini, wazee, vijana kumiminika katika kibanda chake cha kuuza hio dawa.

Sasa mzee huyu yuko wapi?

Babu wa Loliondo kwa sasa ameacha kazi ya utabibu baada ya kupata mikwanja ya kutosha. Jamaa huyu alipogunduliwa kuwa dawa yake ilikuwa haifanyi kazi ilimbidi kuingia mafichoni ili kuikwepa laana na mikono ya wengi...bila shaka wengi waliumia kwa kumsikiliza tabibu huyu.

Maisha ya zamani ya babu wa Loliondo
Babu sahizi ni mtu wa kulengwa kwa manati coz anamiliki nyumba, ana gari aina ya land rover na anaishi maisha ya kistarehe kuliko ya wengi wanayoishi majirani zake.

Picha tulizozipata katika blog yetu ya bkuHABARI zinamuonyesha babu wa Loliondo akipiga pozi kando ya Land Cruiser yake na pia sebuleni kwake. Cheki photo hapo chini.


Sebuleni kwake...hebu chunguza kule ndani

Akila pozi nje ya jumba lake

Akipiga pozi kando ya gari lake

Babu Wa Loliondo...Maisha Ya 'Kitajiri' Ya Sasa Babu Wa Loliondo...Maisha Ya 'Kitajiri' Ya Sasa Reviewed by Admin on Friday, January 31, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.