Unordered List

Definition List

Justin Bieber Kuhofia Kurudishwa Kwao Canada, Watu Wamemkataa

Tangu mwaka jana Justin Bieber amekuwa mtu wa sarakasi huku akifanya mambo ya kuudhi watu wengi. Baadhi ya mambo ya Justin aliyokuwa akifanya ikiwemo kuendesha gari lake kwa kasi jambo ambalo lilimfanya kufunguliwa kesi mahakamani na baadae Justin kuachiliwa kwa dhamana.

Hata hivyo visanga vyake havikuisha na kuna wakati alionekana akiiba baisikeli, pia ashawahi kuonekana live katika kilabu cha madanguro huku video yake akiwa amelala na kibiriti ngoma kusambaa kwa mtandao na baadhi ya mambo mengine ya kuudhi.

Hayo yote hayakuishia hapo na huu mwaka Justin Bieber amekubwa na kashfa la kutumia mihadarati na pia kusemekana alimrushia jirani yake mayai viza.

Wamarekani waliona tabia za Justin si za kawaida na waliona kuwa staa huyu si kigezo chema kwa vijana na walifanya petition kumrudisha kwao.


Deport Justin Bieber!

Drake Bell, ambaye ni mwigizaji filamu wa marekani alianza petition ya kumrudisha Justin kwao na baada ya siku sita pekee ilitimia kiwango kilichohitajika kumrudisha msanii huyu mwenye miaka 19 kwao Canada.

Kufanya petition nchini Marekani unahitaji sahii 100,000 ili iweze kuangalia na rais na kama itakubalika basi jambo linalohitajika na wananchi litatimizwa.

Katika petition hio imeandikwa kuwa Justin Bieber ni mtu anaetishia usalama wa marekani na pia ni mtu mwenye ushawishi mkubwa.
"...not only threatening the safety of our people but he is also a terrible influence."

Sasa jukumu limebakiwa na rais Obama na serikali yake na wakiona kuwa Justin ni tishio kwa wananchi wake basi hakutakuwa na budi ya kumrudisha Justin kwao.

Wengi hawampendi Justin ikizingatiwa kuwa staa huyu ashawahi kupigwa na chupa akiwa jukwaani.
Justin Bieber Kuhofia Kurudishwa Kwao Canada, Watu Wamemkataa Justin Bieber Kuhofia Kurudishwa Kwao Canada, Watu Wamemkataa Reviewed by Admin on Thursday, January 30, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.