Unordered List

Definition List

AGNESS MASOGANGE ANASWA LIVE NA BWANA WA JACK

Agness Masogange akirusha nyavu haikosi.

Wakati huu imemnasua Jux, bwanake Jack Patrick, Juma Khalid a.k.a Jux.

Kulingana na chanzo kilichowanasua wawili hao, walionekana wakitembea sako kwa bako mitaa ya Sinza Kamanyola jijini Dar.

Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.

Masogange alipohojiwa kuhusu uhusiano wake na Jux alidai “Wala hakuna lolote kati yangu na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni watu wangu wa karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa  tunabadilishana mawazo tu.”

Jux na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata huku kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange wakijiachia kumeibua maswali mengi.
AGNESS MASOGANGE ANASWA LIVE NA BWANA WA JACK AGNESS MASOGANGE ANASWA LIVE NA BWANA WA JACK Reviewed by Admin on Friday, January 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.