Unordered List

Definition List

Bonge La Nyau Atafuta Mwonekano, Amponda Diamond Kwa Mtandao.

Msanii wa Bongo ambaye bado ni mchanga katika sekta ya usanii kwa upate wa umaarufu ameamua kumtemea mate Diamond Platinumz kwa kumwambia aache kashfa. Katika akaunti yake ya Facebook, msanii huyu alimpa makavu Diamond kuwa anapenda kashfa za ovyo.

Tatizo limekujaje?

Katika interviews kadhaa Diamond amekuwa akimponda msanii Ali Kiba kuwa ameisha kimziki natoweza kumfikia kamwe pale alipofika yeye. Tukio la mwisho ni wakati alipohojiwa na kituo cha runinga cha Channel 10 na alikuwa na haya ya kusema:

"Unajua kuna watu hawataki kukubali kama mimi ni zaidi yao kuanzia muziki wangu mpaka maisha yangu, mtu anaulizwa Twitter hivi mkiamua kufanya nyimbo moja na Diamond hamuoni kama itapendeza sana et, anajibu never ever haiwezi kutokea mimi kuimba na Diamond. Badala angekubali apate Kick nimrudishe katika muziki analeta dharau wakati hanipati kimuziki mpaka kipesa. Muziki wake hauna tena soko istoshe nasikia asahivi amejiunga na mfuko mpya wa kutoa mikopo PRIDE unaitwa FAIDIKA NA PRIDE kakopeshwa kajenga nyumba. Sitaki kua mnafiki namuweka wazi ni Ali kiba"
Hivi Bonge La Nyau ana haki ya kumpa makavu ama aache muvi iendelee!!
Bonge La Nyau Atafuta Mwonekano, Amponda Diamond Kwa Mtandao. Bonge La Nyau Atafuta Mwonekano, Amponda Diamond Kwa Mtandao. Reviewed by Admin on Sunday, January 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.