Kumekuwa na stori tofauti tofauti kuhusu harusi ya Kimye hasa magazeti mengine yakiongea vibaya kumhusu Kim (New York Post). Hakuna ukweli unaodhihirika.
Lakini tujuavyo ni kuwa Kim Kardashian aliweza kusema 'Ye! kwa Kanye West.
Kulingana na kurasa sita kutoka kwa gazeti hilo, harusi hio ilifanywa siku ya Jumamosi jijini Florence.
Haya ni baadhi ya mambo yaliyofanyika siku hio.
1. Kimye waliweza kufanya harusi juu ya mlima katika jumba la kifalme la Forti di Belvedere.
2. Bafu za kujisaidia ziliekezwa ndani ya boksi lenye urefu wa futi 49 kando na dinner tables. Waitaliano wameipa jina seti hio kama 'Gold Toilet Tower'
3. Ile meza yenye urefu wa mita 40 iliweza kuchongwa majina ya kila mgeni sehemu yake ya kukalia.
4. Masanamu 30 yaliyo uchi yaliekezwa katika meza hio ajab! ili kupamba sehemu yote nzima.
5. Kanye aliondoa taa 80 ambazo zilikuwa zikizunguka katika dance floor. Ilichukua siku 4 kuziandaa.
6. Kanye anaaminika kusema kuwa yeye ndie mtu wa kuangaliwa. Hao wageni wengine si lazima wawekewe taa. " Im the centre of this party, and im the only one person need to see..."
7. Sound System yenye gharama ya $ 136,000 ilitumika na Kanye na iPod yake.
8. John Legend aliweza kukalia piano spesheli ilitengenezwa na mawe.
9. Jaden Smith alivalia nguo ya batman, ulevi ulimfanya kuzunguka kama mjinga kuanzia sa mbili unusu hadi saa nne unusu huku akivunja chupa na glesi.
10. Kim Kardashian aliwasili dakika 25 kuchelewa katika harusi.
11. Mama mzee alianguka baada ya kuzidiwa na kileo, shabiki wa Justin Bieber alianguka kutoka kwa mlima kabla kupelekwa hospitali.
12. Msanii Andrea Bocelli ambaye ni kipofu alifanya shoo yake bila kupewa kiti. Alipomaliza tu aliambiwa ni wakati wake wa kutoka na kuenda nyumbani.
13. Jay Z alimzawadia Kanye na chupa kubwa ya Chianti iliyochopekwa kwa dhahabu iliyoweka diamond badala ya kifuniko.
14. Kim na Kanye waishi na furaha milele?
Kama ulikosa picha official za wawili hawa toka kwa E! Unapitwa.
Pia baadhi ya picha kutoka kwa wageni wa Kimye ikiwemo Jaden Smith, Kendall Jenner na wengine.
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano