Unordered List

Definition List

Picha Za Harusi Za Kim Kardashian Hizi Hapa!

Picha kutoka wedding ya Kim Kardashian ziko hapa!!!

Picha zenyewe za harusi si rahisi kupatikana kwani zinagharimu mamilioni ya madola na Kimye wanapania kuziuza kwa magazeti ya udaku hivi karibuni.

Picha hizi si za kutoka harusini bali ni picha ambazo zimepigwa katika photo booth huko Florence, ikiwapatia wageni wa Kimye nafasi nzuri ya kupiga picha na bibi na bwana kimtindo.

Wale ambao walivuja picha hizi kupitia mtandao wa Instagram ni ikiwemo mwanamziki Tony Williams, designer Tracey Mills na mmoja wa familia Kendall Jenner...Hebu cheki picha zenyewe:

Kim na Kanye wameweza kupata nafasi ya kupiga picha na marafiki
Kimye na marafiki, furaha iliyoje
Khloe Kardashian na Tony Williams, nani mjinga!?
Kendall Jenner photos, aliweza kuzigawa kwa Instagram yake
Tony Williams na Jaden Smith
Kim, Joe na Abbey
Tony Williams na Kimye


 Baadhi ya mambo yaliovuja kuhusu harusi yenyewe ni ikiwemo:
  • Nyimbo ya kwanza ya Kimye kucheza ilikuwa ya John Legend "At Last"
  • Beyonce hakuweza kuhudhuria harusi yenyewe lakini alituma salamz za dhati kupitia Instagram
  • Nguo zote mbili za Kim, Tuxedo ya Kanye West na North West zilitengenezwa na Givenchy
  • Vyakula vilivyoliwa vikiwemo pasta, ricotta cheese; monkfish filet, aromatic herbs; beef filets, potato tarts na truffle green beans (aaaah wapi huku kwetu bora mpunga tu watosha, vyakula vingine tusivyovijua ni gharama)
  • Rob Kardashian aliweza kukosana na familia yake ikabidi arudi zake kabla harusi yenyewe, hakuhudhuria
Endelea kuitembelea TBB upate stori zaidi kuhusu ndoa ya Kimye, picha, video na zaidi zote ambazo zinatokana na mtandao.
Picha Za Harusi Za Kim Kardashian Hizi Hapa! Picha Za Harusi Za Kim Kardashian Hizi Hapa! Reviewed by Admin on Sunday, May 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.