Kufikia sasa wafahamu kuwa Kim Kardashian na Kanye West wameweza kufanya harusi ambayo imehudhuriwa na makumi ya mastaa na mamia ya mapaparazi.
Cha kushangaza ni vile jinsi wawili hawa wameweza kuiweka harusi yao siri ingawa ulimwengu mzima ulikuwa macho kufuatia mambo yao.
Hivi tunavyoongea Kimye waliweza kuepuka mapaparazi wote nchini Italia na chanzo flani kinadai kuwa wawili hawa wako nchini Ireland kwa honeymoon ya siku tano.
Chanzo kinaendelea kusema kuwa wawili hawa waliweza kupaa angani hadi Ireland siku ya jana na baada ya hapo wanatarajiwa kuhudhuria harusi ya rafiki yao ambayo itafanyika Prague.
Baada ya hapo hakuna ajuae watasafiri wapi lakini cha kusema ni kuwa wana muda mrefu wa kuzuru sehemu nyingi. Maybe hata wanaweza kutoklezea huku kwetu
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano