Wiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya showlakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya na msanii Iyanya wa Nigeria.
Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond sasa hivi ambapo amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia kwenye levo za kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho cha kimataifa lakini haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena video Tanzania’ Namkariri Tale akisema ‘video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa sababu tulikua tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake Uingereza ndiomaana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo tutafanya Nigeria tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa kufanya video Tanzania tutafanya hivyo’
Bab Tale: ‘kiukweli tunaumia, tunaumia kwasababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu kama kwenye hii video ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga mpaka milioni 40 za Kitanzania, bado usisahau tumewatoa kina Iyanya Nigeria kwa hela yetu kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class kwenye ndege na hoteli hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa Manzese’
Kwenye sentensi nyingine, Babtale ameithibitishia kwamba Diamond atasikika tena kwenye kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV Afrika.
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano