Je uko tayari kwa video mpya ya 'Subira' kutoka kwa msanii Shaa?
Kama kawaida ya mwanadada huyu, anajulikana kutoa video bomba za kuwaridhisha mafans wake kwa uhakika. Video yake ya awali ya Sugua Gaga iliweza kuvunja rekodi Tanzania kuwa video ya kwanza kabisa kutizamwa mara nyingi kwa mtandao wa Youtube kwa muda mfupi kabla video yenyewe kupigwa marufuku.
Katika video hii mpya, mambo yaonekana ni yale yale.
Shaa ameweza kurusha maandalizi ya video hii kwa AyoTV kutupatia taswira kamili iliyofanyika siku ya 18 Mei wakati wa maandalizi wa video yenyewe.
Kwa kutulambisha tu, Shaa ameweza kutuonyesha madansa wake wakijisheua kwa midundo ya kutamanisha, kuonyesha kuwa video hii itakuwa ya ajab!
Kile ninachosema ni kuwa HATUWEZI KUINGOJEA ZAIDI!!!
Cheki maandalizi ya video yenyewe:
Shaa Atulambisha Video Mpya Ya 'Subira'. IMETISHAAAA!
Reviewed by BkuHabari Admin
on
Monday, May 19, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano