Mchezo wa mashindano ya kuimba ya Tusker Project Fame umesitishwa.
Kulingana na kampuni ya EABL, kipindi hiki ambacho kinaangaliwa zaidi Afrika Mashariki kimeamuliwa kusitisha baada ya EABL kupata hasara wakati wa kukiendesha kipindi hiki.
Na badala yake kipindi kipya cha Tusker Twende Kazi ndicho kitachukua nafasi yake. Kipindi hiki kinashirikisha msanii maarufu na mashabiki ambao wanasafirisha chupa ya Tusker dunia nzima hadi sehemu inapolengwa.
Kulingana na uvumi uliozagaa ni kuwa EABL ilipata hasara katika TPF 6 kwa sababu kipindi hicho hakikuwaridhisha baadhi ya mashabiki.
Inakisiwa kuwa EABL ilikuwa ikigharamika Ksh 200 milioni kwa kila awamu ya TPF ambazo kwa ujumla zilifikia zaidi ya bilioni.
Kipinda cha Tusker Twende Kazi kinatarajiwa kuendelea season mwaka kesho.
Tusker Project Fame Imekufa, Kampuni Ya Bia Ya EABL Yajiondoa
Reviewed by BkuHabari Admin
on
Friday, May 23, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano