Unordered List

Definition List

Agness Masogange Ni Mja Mzito, Avishwa Pete Ya TShs. 16 Milioni Na Mpenziwe

Hakuna ubishi kua Agness Masogange ndio Video Queen maarufu zaidi hapa Bongo, ametokelezea katika video mbalimbali hapa Bongo lakini iliyomtoa zaidi na kumpa jina la Masogange ni video ya Belle9.

Uzuri na umbo lake linawaingiza katika matamanio mengi wanaume walafi lakini kwa inavyosemekana Agness ana wake. Umaarufu wake uliongezeka zaidi pale alipokamatwa na madawa huko Afrika Kusini, jambo lilomfanya anyee debe kidogo kabla ya kuachiwa na kurudi uraiani kwa mbwembwe zote.

Ikapita miezi michache akarudi bongo huku akiwa mtu huru kabisa.Wiki chache zilizopita Agness aliamua kurudi Sauzi kwa yule mchumba wake aliyekoswa koswa kukamatwa nae na madawa ya kulevya na tetesi zinasema kua alirudi Sauzi kumpa taarifa bwana wake huyo kua yeye kwa sasa ni mjamzito.

Tetesi hizo zimethibitishwa jana pale Agness alipoamua kuweka picha yake Instagram na kuandika " Mama Kijacho " Ikimaanisha kua siku si nyingi ataingiza kiumbe kipya duniani.

Inadaiwa kua Mchumba wake huyo kwa furaha aliyoipata baada ya kupewa taarifa hizo aliamua kumvalisha pete ya uchumba kabisa.

Habari BongoClan tulizozipata kutoka kwa ndugu wa karibu wa Agness ambae hakutaka kutajwa jina lake ni kua  Mchumbawake huyo anaplan za kuja Bongo kutoa mahari kabisa ili baada ya Masogange kujifungua wafunge Pingu za maisha. Ndugu huyo aliendelea kusema kua pete yauchumba aliyovalishwa Masogange ina gharama ya shilingi milioni 16 za kibongo.

Tunapenda kutoa hongera kwa Agness na mchumba wake kwa kuamua kuchukua maamuzi mazuri ya kupata mtoto kwani mastar wengi wanaogopa kuazaa kwa kuhofia kushuka umaarufu.

BongoClan

Agness Masogange Ni Mja Mzito, Avishwa Pete Ya TShs. 16 Milioni Na Mpenziwe Agness Masogange Ni Mja Mzito, Avishwa Pete Ya TShs. 16 Milioni Na Mpenziwe Reviewed by Admin on Tuesday, May 27, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.