Unordered List

Definition List

Johani: Ndoa Ya Chuchu Hans Na Ray Kigosi Ni Ndoto

 
Uvumi ulikuja kusikika kuwa ndoa ya Chuchu Hans na Ray Kigosi haidafanyika na sasa madai mengine yamejitokeza kuwa ndoa hiyo ya wawili hao ni kama ndoto.

Blandina Chagula ‘Johari’, juzikati alifunguka kwamba watu waachane na kusikiliza habari za matapeli wa mapenzi, maana suala la Vicent Kigosi ‘Ray’, kumvisha pete mchumba wake wa sasa Chuchu Hans si la kweli na kwamba huo ni utapeli

Akizungumza Ijumaa Mei 13, mwaka huu Johari alisema hana taarifa zozote za Ray kumvisha pete Chuchu na wala hatarajii kusikia tukio la wawili hao kuoana limefanyika.

“Mmh…unasema Ray kamvisha pete Chuchu...! Hakuna jambo kama hilo wewe, achana na matapeli maana hakuna ishu kama hiyo na Ray hawezi kuoa kwa muda huu.”

“Kwani suala la kumvisha pete na kutoa mahari lilifanyikia wapi maana kama kweli kuna mazingira hayo basi atakuwa kafanya kwa kificho sana.”
Na Musa Mateja, GPL
Johani: Ndoa Ya Chuchu Hans Na Ray Kigosi Ni Ndoto Johani: Ndoa Ya Chuchu Hans Na Ray Kigosi Ni Ndoto Reviewed by BkuHabari Admin on Friday, May 16, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.