Ni wiki kadhaa zilizopita ambapo Diamond alizungumza exclusive na DStv.com na kusema atakua na safari ya Uingereza. Tayari time imetimia ambapo usiku12 May 2014 waliondoka kuelekea UK akiwa na rafiki yake Ommy Dimpoz ambae pia alifanya video yake mpya huko huko na bado haijatoka.
Diamond amekwenda kushoot video yake mpya ya moja kati ya nyimbo mbili atakazozitoa hivi karibuni huku akisisitiza kwamba mpango wake ni kutoa nyimbo mbili mbili kila anapofikiria kuja na mpya.
Anasema wimbo mmoja utakua kwa ajili ya Afrika Mashariki na mwingine utakua kwa ajili ya Afrika kwa sababu imekua ngumu kwa wana Afrika Mashariki kuzielewa touch za Magharibi zikifanywa na mtu wa East Africa.
Mr. Moe Mussandio anaetajwa kupewa nafasi ya Diamond kwenye hiyo video mpya akiwa tayari ameshafanya kazi na Ommy Dimpoz kwenye video yake mpya ya Davido Skelewuna nyingine za mastaa kama Wizkid na FUSE ODG.
Bado haijajulikana jina la wimbo huo mpya wa Diamond lakini endelea kukaa karibu na dstv.com stori ikitoka itakufikia hapa.Diamond, Davido na Wizkid wote wapo kwenye nomination mbali mbali za MAMA. Wapigie kura katika www.mtvbase.com kabla 4 June.
Stori na Millard Ayo
Chanzo dstv
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano