Harusi ya Kim Kardashian na Kanye West inatarajiwa kufanyika mwezi huu tarehe 24 na wanaotarajiwa kuhudhuria ni watu watajika na inakisiwa idadi kuwa 100.
Harusi hii ambayo itafanyika Varsailles jijini Paris inapaniwa kuleta mikwanja mikubwa.
Harusi ya awali ya Kim na Humprey japo ilikuwa ndoa ya siku 72 pekee waliweza kupata milioni $18. Hivi sasa duru zinasema kuwa Kim Kardashian ana ajenda ya kuongeza pesa hizo katika harusi yake ya tatu na Kanye.
Kulingana na jarida la In Touch, Kim yuko mbioni kuhakikisha kuwa ameweka rekodi ya kupata hela zaidi ya milioni $20 huku akitumia mbinu zozote ili kufaulu.
Milioni $15 zinatarajiwa kutoka kwa runinga ya E! ambayo inasimamia harusi hio na wenye hakimiliki katika hio harusi.
Halafu pia wakati wa harusi hio watu hawatoruhusiwa kushoot kamera yeyote isipokuwa E! wenyewe.
Pesa myingine zinazotarajiwa ni kutoka kwa gazeti la Vogue baada ya kufanya mauzo ya picha za harusi za Kimye.
Pia Kim atapunguza ngarama ya chakula kwani wahisani watatoa vyakula vya bure kujitangaza.
Kiufupi hii harusi itakuwa ya juu.
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano