Unordered List

Definition List

Je, Ulikuwa Wajua Kuwa Wanaume Wenye Sauti Nzito Huwavutia Wanawake?

Vin Diesel
Ushawahi kujiuliza kwa nini Vin Diesel anawavutia wanawake wengi? Wengine wanaweza kusema kusema kuwa ana sura nzuri ya kupendeza, lakini itakuwaje kuwa wanawake ulimwengu mzima wanavutiwa na mwigizaji huyu? Ama ni sauti yake nzito? Kulingana na utafiti mpya uliofanywa nchini Canada, hii ndio inaweza kuwa sababu kuu.

Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wenye sauti nzito wana kipao mbele cha kuwavutia wanawake kulingana na utafiti ulioandikwa kwa 'Personality and Individual Differences'.

Baada ya utafiti kufanywa kwa wanawake kadhaa ambao waliambiwa wachague sauti ambazo zilijeuzwa toni tofauti tofauti za wanaume, ilionekana kuwa wanawake walipendelea sauti nzito.

Cha kushangaza ni kuwa watafiti waligundua kuwa wanaume wenye sauti nzito mara nyingi hudanganya katika ndoa lakini vivyo hivyo wanawake waliotafitiwa waliwaona kama wanavutia.

Mpaka sahizi haijajulikana ni kwa nini wanawake wangependa kuwa katika mahusiano na wanaume wenye sauti nzito ambao watawadanganya kulingana na utafiti wa Jillian O' Connor, uliona kuwa wanawake walijua kuwa wanaume hao hupenda kudanganya, ndipo wanazidi kuwapenda kwa sababu mahusiano yao hayatakuwa marefu.
Je, Ulikuwa Wajua Kuwa Wanaume Wenye Sauti Nzito Huwavutia Wanawake? Je, Ulikuwa Wajua Kuwa Wanaume Wenye Sauti Nzito Huwavutia Wanawake? Reviewed by Admin on Saturday, January 04, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.