Unordered List

Definition List

RELAX, RAY C BADO YUPO SINGLE

Sasa waweza kupumua vyema kwani Ray C ameweka wazi kuwa yuko single.

Ray C alizuwa wasiwasi mkuu bale alipoweka picha yake na jamaa aliyedai ni mpenziwe, jambo ambalo halikuchukuliwa vyema na mashabiki wake ambao wanammezea mate.

Akiongea na Bongo5, Ray C amesema picha alizoziweka Instagram akiwa na mwanaume si maisha halisi bali alitaka ‘kuhave fun’ na mashabiki wake. Lakini amekiri kuwa usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume si mdogo.

“Sijapata bado mchumba nilikuwa nawachombeza fans wangu kwenye Instagram kwasababu nasumbuliwa sana.”

Kuhusu nyimbo mpya, Ray C amesema mwaka huu atarudi kwenye muziki kwa kuachia nyimbo mfululizo akianza na ‘Walimwengu Wote Wajue’utakaotoka mwezi March.

“Wapenzi wa muziki wangu wakae mkao wa kula,nyimbo zipo tayari bado kuziachia tu. Mwaka huu nitaanza na wimbo ‘Walimwengu Wote Wajue’ ambao umefanyikia chini ya C9 Records. Baada ya hapo harakati za muziki zitaendelea,” alisema Ray C.

Katika hatua nyingine, Ray C ameandika ujumbe huu kwenye Instagram: Yes am back……Ingawa wabaya wangu walitamani nisipone…Mungu alinipenda zaid…back to life ….am back Yo!!!Sty Tuned….Big Things r
coming.
RELAX, RAY C BADO YUPO SINGLE RELAX, RAY C BADO YUPO SINGLE Reviewed by Admin on Wednesday, January 08, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.