Unordered List

Definition List

Diamond Platinumz Atetea Ngozi Mpya Ya Wema: Imekuwa Nzuri Yenye Afya!

Wema Sepetu
Mitandao ya kijamii ilikurupuka kwa muda mrefu baada ya kufahamika kuwa Wema Sepetu alibadilisha ngozi wakati alipokuwa nchini Uchina. Ilikuwa kizaa zaa na haikuwa rahisi kwani ilikuwa aibu kuu kwa msanii huyu wa Bongo Movies.

Lakini sahizi kuna afueni kidogo baada ya Diamond kufunguka rasmi na kumtetea Wema kuhusu ngozi yake mpya. Akiongea na gazeti la Michezo, staa wa Number One Diamond Platinumz alidai kuwa anaipenda ngozi mpya ya Wema Sepetu.

“Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani,  ameacha kabisa kutumia dawa za
kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani alisikiliza ushauri niliompa kabla.”


Kama hujajua basi ni kuwa Diamond na Wema wamerudiana rasmi mwishoni mwa mwaka jana na Diamond ameapa kuwa na Wema hadi kifo kitakapowatenga....na kuhusu uzao wake na Wema bado ni uleule. Diamond aliogezea akigusia uzao wake na Wema:

“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.”
Diamond Platinumz Atetea Ngozi Mpya Ya Wema: Imekuwa Nzuri Yenye Afya! Diamond Platinumz Atetea Ngozi Mpya Ya Wema: Imekuwa Nzuri Yenye Afya! Reviewed by Admin on Saturday, January 04, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.