Unordered List

Definition List

Agness Masogange Anaswa Akidengua Kiuno Kwa Nisha

BAADA ya kujificha muda mrefu tangu atoke mahabusu nchini Afrika Kusini kwa msala wa madawa ya kulevya, Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’ amenaswa ‘live’ akikata mauno huku akipewa kampani na mtoto mdogo nyuma yake.

Weekly Star Exclusive  ilimbamba mrembo huyo juzikati nyumbani kwa mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar ambapo Nisha alikuwa akipiga makofi na kushangilia wakati Masogange alipokuwa akikata mauno.
“Sijacheza siku nyingi jamani ndiyo maana leo nimejikumbushia mambo yangu ya mjini, kuna vitu vingi sana nilivimisi kama kukutana na watu hivi na kucheka pamoja kwa uhuru,” alisema Masogange.
Wakati akiendelea kukatika, mtoto mdogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja mwenye umri uliokadiriwa kama miaka 7, alishangilia na kucheza naye pamoja.
Tangu arejee kutoka Bondeni, Masogange amekuwa shosti mkubwa wa Nisha ambapo mbali na urafiki, wanafanya filamu pamoja iitwayo Betina na Zena.
Kwenye msala wa madawa ya kulevya, Masogange aliachiwa kwa kulipa faini baada ya kuthibitika kuwa mzigo aliokutwa nao haukuwa madawa ya kulevya bali ni ‘material’ ya kutengenezea madawa tofauti.
Agness Masogange Anaswa Akidengua Kiuno Kwa Nisha Agness Masogange Anaswa Akidengua Kiuno Kwa Nisha Reviewed by Admin on Saturday, January 04, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.