Unordered List

Definition List

Aunt Ezekiel Akiri Kuwa Mumewe Alishikwa Nchini Dubai

Stori Na Hamida Hassan
STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekiri mumewe kukamatwa na kupata misukosuko lakini si kufungwa kama baadhi ya watu wanavyoeneza uzushi.

Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema mumewe, Sunday Demonte alikamatwa kutokana na viza yake kuisha ambapo alishikiliwa kwa muda na alipokamilisha taratibu za ‘kurinyuu’, aliachiwa.
“Nashangaa sana mambo haya yamevuma kuwa mimi nimemuacha mume wangu amefungwa, ukweli ni kwamba mume wangu yuko huru na hata sasa ukitaka ongea naye, ni mwanamke gani atakuwa na furaha hivi wakati mumewe ana matatizo?” alihoji Aunt.

Katika mistari mingine, Aunt alisema watu wengi wanatamani kuona ameachika au kujua mwenendo wa maisha yake na mumewe lakini wanajidanganya kwani yeye ni mwanamke aliyeamua kuolewa na amefundwa hivyo wataambulia patupu.
“Siyo  rahisi mimi kutoa siri ya maisha ninayoishi na mume wangu, ni makubaliano yetu. Kimsingi ndoa yetu iko imara, watasubiri sana na watachoka wenyewe,” alisema Aunt.
Aunt Ezekiel Akiri Kuwa Mumewe Alishikwa Nchini Dubai Aunt Ezekiel Akiri Kuwa Mumewe Alishikwa Nchini Dubai Reviewed by Admin on Thursday, January 02, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.