Unordered List

Definition List

Mwaka Wa Majanga Kwa Snura?!?

Huku staa wa kupiga mauno Snura kupigwa marufuku nyimbo yake ya Nimevurugwa kutochezwa katika runinga za nchini, sasa amefunguka kuwa ugonjwa wa presha unamsumbua sana.

Staa huyu amekiri kuwa hajui tatizo gani linamsumbua kwani kila wakati akienda hospitalini anaambiwa kuwa presha imepanda na pia vidonda vya tumbo.

“Nimekuwa nikiumwa mara kwa mara na nikishikwa ni lazima niwekewe drip kwani naishiwa nguvu nakosa raha pia, sijielewi ingawa naambiwa kuwa nina mawazo,” alisema Snura akiwa nyumbani kwake, Mwananyamala, jijini Dar.


Mwaka Wa Majanga Kwa Snura?!? Mwaka Wa Majanga Kwa Snura?!? Reviewed by Admin on Tuesday, January 28, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.