Unordered List

Definition List

Wazijua Sababu Za Diamond Platnumz Kumake Headlines Kwa International Awards?


Una habari kuwa kuna sababu zilizompelekea diamond kuzidi ku-make headlines siku hadi siku?, kama ilivyo kwa msanii yeyote yule mwenye mafanikio duniani, kuna ishu mbili tatu zilizowahi kumtokea katika maisha yake, ambazo ndio zilimpelekea kumsukuma, pamoja na jitihada zakujituma, kuweza kumfikisha hadi kwenye mafanikio yake. Kama ulikuwa hujui, basi bila Diamond kufanya haya, hii leo, hizo tuzo zote, kuanzia ya mtv na kili zingekuwa bado ni ndoto, na kwa hapa Tzee angekuwa na-hit tu kinyumbani nyumbani kama ilivyo kwa wasanii wengi wa bongo fleva.

Rumors has it kwamba, bila Diamond kugombana na aliyekuwa manager wake wa zamani, hii leo asingekuwa amefikia hapa alipo, manyanyaso aliyoyapata hapo nyuma, akiwa na uongozi wake wa zamani, ndio iliyomsukuma kufanya vitu kwa bidii na kufikia hadi hii leo, mbali na struggle zake za kila siku katika kujitangaza kimuziki.

Inasemekana kuwa management yake ya sasa ndio inayompa sapoti kubwa sana katika kufanya vitu ki-international zaidi, na jina lake kuzidi kukua ulimwenguni, hadi kwa hivi sasa watu wameshamsahau Diamond wa mbagala.


Kama ilivyo katika kila biashara, bila risk huwezi kupata kile ulichokuwa unatarajia, na wala huwezi kuendelea, utabaki hapo hapo siku zote, hii ndio mchezo aliofanya Dangote, kuanzia kutoka kufanya video za milioni mbili hadi kufikia mahali na kufanya video za zaidi ya milioni ishirini, kitendo hichi ndicho kilichopelekea Diamond Platnumz aweze kujulikana zaidi nchi mbali mbali, haswa kwa nyimbo yake ya “my Number1”. Ni moja kati ya vitu ambavyo matunda yake yanaonekana hadileo, kwa kuendelea kukaa on top kwenye charts, hadi kumpelekea tuzo mbalimbali.
Wazijua Sababu Za Diamond Platnumz Kumake Headlines Kwa International Awards? Wazijua Sababu Za Diamond Platnumz Kumake Headlines Kwa International Awards? Reviewed by Admin on Monday, July 07, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.